Hospitali za mabepari

Ubinafsishaji wa huduma ya afya nchini Kenya.

Photo by Marcelo Leal on Unsplash

Inasemekana kuwa taifa yenye afya ni taifa ifanyayo kazi, lakini katika nchi ambayo huduma ya afya inamilikiwa na watu binafsi na ukosefu wa ajira umezidi, hamna afya wala kazi. Nimeshuhudia haya dada yangu alivyo ugua.

Nilihitimu shahada ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, mnamo mwaka wa 2017. Nikiwa chuoni, niliajiriwa katika kiwanda cha mvinyo (Kenya Wines and Agencies Limited) kama mfanyakazi wa kawaida. Ni nafasi ambayo wafanyakazi wametengwa na bidhaa inayotokana na kazi yao. Tulitengeneza, pakia, na kusambaza mvinyo na vinywaji vingine, lakini wengi wetu walikuwa wanalipwa shilingi mia nne (dolla 4) kwa siku. Vile vile, hatukumudu tunazotengeneza na ni sheria kutiwa mbaroni na kufungwa katika kituo cha polisi cha sehemu ya viwandani ungelipatikana kutumia bidhaa hizo.

Motisha ya uamuzi wangu kusomea shahada ya uchumi katika chuo kikuu ilikuwa kuelewa madogo na makuu ya uchumi yaliyokuwa misingi ya uzalishaji nchini Kenya, na kuboresha hali ya Maisha nyumbani. Kama mkufunzi, matarajio yetu yalikuwa kama kuajiriwa katika wizara ya serikali, benki kuu ama wizara ya hazina. Lakini, baada ya kupewa uwezo wa kusoma, kuandika na kufanya inavyohitajika na shahada yetu, ukweli wa mambo katika ulingo wa ajira ni tofauti kabisa, kwani nafasi za ajira ni nadra nchini ambamo wasomi elfu tisa huhitimu kila mwaka.

Photo by Arseny Togulev on Unsplash

Baada ya kuhitimu, pamoja na matarajio ya familia ya  kuboreshewa hali ya kimaisha, dada yangu, marehemu Winnie Anyango, akaugua Januari 2018. Tulimpata siku tatu baada ya kuzimia nyumbani kwake. Alilazwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta mbapo mdaktari wamkuta kuwa na shida ya mfumo wa neva, kilichozalisha ukosefu wa uratibu miguuni. Alipokea matibabu kwa muda wa miaka miwili na nusu lakini hakupona. Juma ya kwanza ya Mei 2020, alizimia tena akapelekwa hospitali ya St Mary Langata alikokutwa kuwa na uvimbe wa ubongo. Madaktari wa St Mary walipolinganisha MRI iliyofanywa katika hospitali ya Kenyatta na waliyofanya, walipata kuwa uvimbe ulionekana lakini ulikuwa mdogo wakati ule. Hatakama hospitali ya Kenyatta haikuitambua hapo awali.

Matokeo haya yalitupumbaza sana kwa kuwa upasuaji wa ubongo ungehitaji pesa nyingi. Tulijiuliza maswali mengi: tungemudu kivipi matibabu yake? Na angehitaji kusafirishwa ughaibuni kwa matibabu, ingewezekana kweli na huku kusitishwa safari za kawaida kwa jili ya covid-19? Tulifanya kadri ya uwezo wetu kutafuta zile hela za matibabu lakini Winnie aliaga dunia tarehe 28 Mei 2020.

Pamoja na ukosefu wa ajira, nchi yangu inakabidhiwa na ukosefu wa huduma ya afya ilhali wanaojihushisha na ubepari wanamudu huduma bora ya afya. Hata daraja la kati ya kiuchumi wanaofanana na mabwanyenye, wana umbali wa ajali mbaya ya barabarani na ugonjwa mbaya kutoka kwa umaskini. Utambuzi mbaya umeenea sana na watu wengi wamekufa kutokana na magonjwa ambayo yangetibiwa yangelitambuliwa mapema, au kama wangeenda katika hospitali kubwa na ya kibinafsi inayotoza tibabu ghali. Hali huzorota kwa masikini wanaoishi katika makao isiyo rasmi kulingana na matokeo ya utafiti iliyofanywa muda sio mrefu uliopita: Upatikanaji wa huduma bora za afya katika eneo bunge ya Embakasi North. Tulifanya utafiti huu a muda sio mrefu uliopita. Ni vyema kutilia manani matokeo yake hapa:

  1. Zaidi ya vituo vya afya vya kibinafsi hutoza shilingi 10000 (dolla 100) kwa kiwango cha chini kabla ya kumpa mgonjwa matibabu ya dharura na wengi wao wamo hatarini mwa kufa kabla ya kuhudumiwa.
  2. Vituo vya afya vya uma vina ukosefu wa dawa (ambacho ni uvivu wa kimuundo) na wagonjwa wanaelekezwa katika maduka ya dawa jirani kununua dawa ambazo zinauzwa kwa bei ghali.
  3. Vituo vya afya haviwafirikii wanaoishi na ulemavu ambao wanashindwa kutumia vyoo kwa mfano kwani havina miundo ya kuwasaidia.
  4. Umakini kazini katika vituo hivi vya afya umezorota sana. Wafanyikazi wanapiga gumzo badala ya kuwahudumia wagonjwa.
  5. Ukosefu wa madaktari wenye ujuzi wa kitaaluma ambacho husababisha utambuzi wa kimakosa.
  6. Vituo vingi vya afya havina huduma za maabara .
  7. Ukosefu wa ujuzi pamoja na huduma za kupanga uzazi au huduma za afya ya kimapenzi . Hivi sasa, vijana wa umri wa miaka 12 wanajihusisha kimampenzi bila kutumia kinga na wamo hatarini mwa magonjwa ya zinaa, ubakaji, mimba za mapema , na ukatili wa kijinsia. Ni muhimu kunakili kuwa mmoja kati ya wasichana watano walio na umri wa 15-19 ni waja wazito au wamejifungua. Hali hii huchangia pakubwa kuavya mimba kwa njia isiyo halali kiafya na kisheria hivyo kuhatarisha maisha yao. Kwa hivyo ni muhimu kupunguza umri wa wasichana kuhalalisha kufunzwa afya ya kimapenzi ili wafanye uamuzi mwema ulio na ujuzi.
  8. Sheria za kiislamu zinahitaji wagonjwa wa kike wahudumiwe na madaktari wa kike na wanaume wahudumiwe na madaktari wa jinsia yao. Katika hospitali nyingi kanuni hii haizingatiwi katika kutoa huduma za afya.
  9. Ujuzi wa kitaaluma umekosekana katika vituo vya afya vya umma. Wauguzi na madaktari hutumia lugha chafu na wajawazito wanapigwa wakijifungua.
  10. Mwisho, hatuna dawa za kutosha kwa wajawazito katika vituo vya afya vya umma. Wanalizimshwa kujinunulia dawa nje ya vituo hivi.

Kwa minajili ya kuzidisha mapato, ubepari umewapora wananchi wa kawaida mahitaji ya kimsingi ambayo ni muhimu kwa kuishi.  Kwa hivyo ni jukumu letu kama wanaharakati wa haki za kijamii katika vituo vya haki za kijamii kueneza elimu ya kisiasa na kudai huduma bora ya afya, makazi, chakula, maji safi na uchukuzi wa taka, elimu bora ya bure, ajira na heshima kwa haki za kibinadamu na utu kati ya haki zingine nyingi. Kumalizia, Dedan Kimathi alisema “ ni bora kufa kwa miguu yangu kuliko kuishi kwa magoti,” na mwishowe watu wenyewe watainuka ili kujikomboa. Ili kuwa taifa yenye afya inayofanya kazi, ni jukumu letu kudai ajira bora na huduma ya afya zaidi.

Further Reading